EWURA YATOA BEI MPYA YA MAFUTA

 


Bei za mafuta nchini Tanzania zimepanda mwezi huu Aprili ikilinganishwa na mwezi Machi 2024.

Katika Jiji la Dar es Salaam mafuta ya petroli yamependa kutoka Tsh. 3,163 mwezi Machi hadi 3,257 kwa lita huku dizeli ikiongezeka kutoka Tsh. 3126 hadi 3,210 mwezi Aprili.

Mamlaka ya udhibiti wa huduma ya Nishati na maji Ewura imesema kwamba ongezeko hilo la bei limechangiwa na kuongezeka kwa bei ya mafuta yaliosafishwa katika soko la dunia, mbali na ongezeko la kiwango cha kubadilisha fedha za kigeni kwa asilimia 3.19 kutokana na ongezeko la matumizi ya Euro kulipia mafuta yalioagizwa.

Bidhaa hiyo pia imeongezeka bei katika miji ya Tanga , na Mtwara ambako itauzwa kutoka Tsh. 3,209 hadi Tsh. 3,303.

Post a Comment

0 Comments