GAVANA TUTUBA AMEFANYA MAZUNGUMZO NA UJUMBE WA SHIRIKA LA MILLENIUM CHALLENGE
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Emmanuel Tutuba amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Shirika la Millenium Challenge (MCC) ukiongozwa na Bw. Bradley Cunningham na kujadili mambo mbalimbali kuhusu upatikanaji wa huduma za fedha nchini na uwepo wa mazingira rafiki ya uwekezaji na biashara ambayo ni nyenzo muhimu katika  ustawi wa sekta ya fedha.


Kikao hicho kilichofanyika katika ofisi za Makao Makuu Ndogo ya BoT, Dar es Salaam, kilihudhuriwa pia na Naibu Gavana (Sera za Uchumi na Fedha), Dkt. Yamungu Kayandabila, na maafisa wengine waandamizi wa BoT.


Post a Comment

0 Comments