IBUENI FURSA ZA KIUCHUMI KUONGEZA MAPATO YA HALMASHAURI

 OR-TAMISEMI, MWANZA


Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bwana Balandya Elikana amewataka Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata kubuni na kuibua vyanzo vya mapato kwa mustakabali wa maendeleo ya Halmashauri zao. 


Akifungua Mafunzo kwa Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata Mkoa wa Mwanza leo tarehe 28 Aprili, 2024 katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw. Balandya Elikana amesema mojawapo ya changamoto zinazozikabili Mamlaka za Serikali za Mitaa ni makusanyo haba ya mapato ambayo suluhisho lake ni ubunifu wa vyanzo vya mapato ambavyo kimsingi vinapatikana katika ngazi ya msingi na maafisa hao wanayo dhamana ya kutekeleza jukumu hilo.


“uzoefu umeonesha kuwepo kwa changamoto za kukosa ubunifu wa uibuaji wa fursa za kiuchumi na kijamii zinazopatikana kwenye ngazi za msingi pamoja na ushirikishwaji wa wananchi na Wadau wa Maendeleo hivyo ni matarajio yetu kwamba mtakusanya mapato kutoka katika vyanzo mbalimbali na kufanya usimamizi wa makusanyo ili kufikia malengo ambayo Halmashauri imejiwekea” alisema Bw. Balandya Elikana.


Aidha, amewataka maafisa hao kuwa kiungo kati ya Serikali Kuu na wananchi katika Tarafa, kushiriki na kutoa ushauri kuhusu upangaji wa mipango ya maendeleo kwenye maeneo yao pamoja na kuandaa Mpango Kazi wa Maendeleo na kuuwasilisha kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ili utekelezaji uwe wa pamoja.


Naye Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Tawala za Mikoa Bw. Ibrahim Minja amesema matarajio ya mafunzo hayo ya siku mbili ni kwenda kuwasadia Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata kutatua kero na malalamiko ya wananchi katika ngazi za msingi. 


Aidha, Minja aliongeza mafunzo ni awamu ya tatu inayohusisha mikoa ya Simiyu, Mara, Mwanza, Kagera na Geita ambayo itafikisha idadi ya mikoa 18 iliyopata mafunzo na kubakia mikoa 6 ambayo pia maafisa wa kada hiyo watapatiwa mafunzo kabla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024.


Kwa upande wake Gaudensia Venance Mtendaji wa Kata ya Kirumba Jiji la MwanzaPost a Comment

0 Comments