IDARA YA AFYA WATEKELEZA MAAGIZO YA WAZIRI MCHENGERWA

 IDARA YA AFYA WATEKELEZA MAAGIZO  YA WAZIRI MCHENGERWA


Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Rashid Mfaume amefika wilayani Rufiji na Kibiti kukagua na kufanya tathmini ya uharibifu wa miundombinu ya Afya iliyoharibika kutokana na Mafuriko.


 Akizungukq baada ya kukagua Kituo cha Afya Mohoro, Kata ya Mohoro wilayani amesema wamefika kituoni  hapo kutekeleza maagizo ya Waziri Mchengerwa, ambaye aliwataka kufanya tathimini na uharibifu pamoja na mahitaji ya maboresho ya huduma za Afya.


Nimefika Mohoro nimejionea namna ambavyo Kituo cha Afya pamoja na nyumba sa watumishi  zimezingirwa na maji kuwa Kituo cha Afya Mohoro zimezingirwa na maji kutokana na hali hii kuna kila sababu ya kujenga kituo Cha Afya katika eneo lingine ambalo tayari limeshatengwa ili kuiwezesha jamii kuendelee kupata huduma ya matibabu.


"Sasa tumeshafanya maamuzi, eneo limeshatengwa tutakachokifanya ni kuharakisha upatikanaji wa fedha ili ujenzi uanze." Aliongeza Dkt. Mfaume.


Awali Mganga Mkuu wa Wilaya  Dkt. Hamisa Abdallah alisema Kabla ya kufunga  Kituo hicho kilikuwa kikitoa huduma kwa Watu 22, 000 ambapo Kwa Sasa wamelazimika kuhamisha kituo hicho katika eneo la muda.Katika hatua nyingine akiwa kituo Cha Afya Mloka Wilayani Rufiji mkoani Pwani Dkt. Mfaume amemtaka Mganga Mkuu wa Mkoa kushirikiana na Mganga Mkuu wa Wilaya kuhakikisha majengo yaliyokamilika yanaanza kutoa huduma Kwa Wananchi na kuweka utaratibu wa kumpata mtaalamu wa usingizi Ili kituo hicho kianze kutoa huduma za upasuaji pamoja na matumizi ya maabara ya kisasa iliyojengwa na Serikali.

Post a Comment

0 Comments