INTER MILAN YAMTAKA ANTONY MARTIAL

 


Inter Milan wanaweza kumnunua fowadi wa Ufaransa Anthony Martial wakati kandarasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 na Manchester United itakapokamilika msimu huu wa joto - ikiwa watashindwa kumsajili mshambuliaji wa Iceland Albert Gudmundsson, 26, kutoka Genoa . (Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)

Brighton hawana nia ya kumnunua tena Ansu Fati baada ya uhamisho wake wa mkopo kutoka Barcelona lakini Wolves , Valencia na Sevilla wanawezakuwasilisha ofa kwa mshambuliaji huyo wa Uhispania, 21 msimu huu wa joto. (Sport - kwa Kihispania).

Everton itahitaji zaidi ya pauni milioni 40 ili kumuuza mshambuliaji wa Uingereza Dominic Calvert-Lewin, 27, msimu huu wa joto. (Football Insider)

Luton wameonyesha nia yao ya kutaka kumnunua mshambuliaji wa Blackburn na Jamhuri ya Ireland Sammie Szmodics lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Brentford (Sun)

Post a Comment

0 Comments