JOKATE NA ABDI KUPOKELEWA KWA KISHINDO ZANZIBAR

 


Na mwandishi wetu

Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa wametangaza Mapokezi Makubwa na ya Kihistoria ya Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo *Ndugu Jokate Urban Mwegelo (MNEC)* na Naibu Katibu Mkuu UVCCM Zanzibar *Ndugu Abdi Mahmood Abdi*, Mapokezi hayo yatafanyika siku ya Jumamosi tarehe 20 April 2024 Afisi kuu Zanzibar kuanzia saa 2:00 Asubuhi.


"Tarehe 20 Aprili, 2024 Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi tunatarajia kuwa na mapokezi makubwa na ya kihistoria kwa viongozi wetu ambayo yatafanyika Afisi kuu za UVCCM Zanzibar. Hii ni siku muhimu sana kwa wanachama na wananchi wote waliopo Zanzibar na  walio tayari kuja Zanzibar kwa ajili ya tukio hili".


"Tunatoa wito kwa wanachama wote na wananchi kwa ujumla kushiriki mapokezi haya kama sehemu ya kuunga  mkono  viongozi wetu hawa ambao ni hodari na wana uwezo na ueledi mkubwa sana wa kifikra na kiutendaji". Ndugu Bulugu Magege KMM-Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa. #Kazi Iendelee

Post a Comment

0 Comments