KAMATI TTSS YAFANYA KIKAO NA GAVANA TUTUBA

 


Kamati Tendaji ya Utafiti wa Sekta ya Utalii Tanzania (TTSS) imefanya kikao chake cha kawaida Ofisi ya Makao Makuu Ndogo ya Benki Kuu ya Tanzania Dar es Salaam tarehe 4 Aprili 2024.


Kikao hicho chini ya uenyekiti wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbas na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, kinawashirikisha wajumbe kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Bodi ya Utalii Tanzania, Ofisi ya Uhamiaji, Ofisi ya Takwimu ya Taifa na Benki Kuu ya Tanzania.


Kikao kimejadili masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya utalii kwa ujumla, ikiwa ni pamoja wasilisho la matokeo ya utafiti wa wageni wa kimataifa waliotembelea Tanzania mwaka 2023.

Post a Comment

0 Comments