KATIBU MKUU UVCCM NDUGU JOKATE MWEGELO AZINDUA KIWANDA CHA ANNO DOMINI FOOD INDUSTRIES MKAONI MTWARA

 

Na mwandishi wetu


Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja Chama cha Mapinduzi Komredi Jokate Urban Mwegelo (MNEC) amezindua Kiwanda cha Kuchakata nafaka Anno Domini Food Industries Mkoani Mtwara tarehe 28 Aprili, 2024.


Mkurugezi wa Kiwanda hicho Ndugu Thobias  Aloyce Mhana amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanua kwa kuweka Mazingira wezeshi kwa Vijana kujiajiri.


Aidha Ndugu Thobias amesema Kiwanda hicho kinaenda Kufungua Fursa kwa Vijana wengi kwani Mpka sasa kimeajiri Vijana 10 na Kikianza kazi Rasmi kitaajiri Vijana Zaidi ya 20.


Akizungumza kwa Niaba ya Jumuiya Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM anayefanyia Kazi zake Zanzibar Ndugu Abdi Mahmoud Abdi amepongeza uwekezaji wa Kiwanda hicho kwani ni fursa kwa Wananchi wa Mtwara hususani Vijana, lakini pia Ndugu Abdi amewaahidi Vijana katika Kiwanda hicho kuwa Changamoto zote walizoziwaailisha wataziwasilisha kwenye Mamlaka husuka kwa ajili ya ufumbuzi.


Ndugu Jokate Urban Mwegelo amewaahidi Vijana hao kuwa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi chini ya Mwenyekiti wake Ndugu Mohammed Ali Kawaida (MCC) milango yake iko wazi wakati wote kuwasemea Vijana aa Kitanzania hivyo wasisite kubisha hodi pale wanapoona kuna Changamoto ya Aina yoyote inayohitaji utatuzi.


#KulindaNaKujengaUjamaa

#SisiNaMamaMleziWaWana

#Kaziiendelee


Imetolewa na; 

Idara ya Uhamasiahaji na Chipukizi UVCCM Taifa.

Post a Comment

0 Comments