LIVERPOOL YAFANYA MAZUNGUMZO NA TRENT ALEXANDER-ARNOLD KUHUSU MKATABA MPYA

 


Liverpool wako kwenye mazungumzo na Trent Alexander-Arnold kuhusu mkataba mpya wa beki huyo wa kulia wa Uingereza, 25. (Football Insider)

Dinamo Zagreb wamelipa tangazo la ukurasa mzima katika gazeti la michezo linalouzwa zaidi nchini Uhispania, Marca, katika jaribio la kumshawishi kiungo wa kati wa Croatia Luka Modric, 38, kurejea katika klabu yake ya kwanza iwapo ataamua kuondoka Real Madrid msimu huu. (ESPN)

Paris St-Germain wamesitisha mazungumzo ya kuongeza mkataba na kakake mdogo wa Kylian Mbappe Ethan Mbappe, 17, huku mkataba wa sasa wa kiungo huyo wa kati wa Ufaransa chini ya miaka 16 ukimalizika Juni. (RMC Sport - in French)

Post a Comment

0 Comments