MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ULINZI INA KILA SABABU YA KUJIVUNIA MAFANIKIO MAKUBWA-DKT SERGOMENA

 


Na mwandishi wetu

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence amesema katika kuadhimisha Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania,.Wizara ya ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa lina kila sababu ya kujivunia mafanikio makubwa yaliyopatikana katika awamu zote sita za uongozi.


Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya Wizara hiyo katika kipindi cha miaka 60 ya Muungano wa Tanzania Aprili 3, 2024 jijini Dodoma amesema miongoni mwa mafanikio ya Muungano ni pamoja na ushiriki wa Wizara kupitia taasisi zake hususani JWTZ katika kukuabiliana na majanga au maafa mbalimabali pale yanapotokea katika kutekeleza jukumu hilo.


Dkt. Stergomena amesema JWTZ imeendelea kushiriki kikamilifu katika kutoa misaada ya uokoaji na ile ya kibinaadamu kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa.Aidha amesema JKT imeendelea kufanya kazi kubwa na nzuri ya kuzalisha mali, kuwapa vijana wa kitanzania mafunzo ya awali ya kijeshi na stadi za kazi, ili kuwajengea ukakamavu, uzalendo umoja wa kitaifa na uwezo wa kujitegemea.


Amefahamisha kuwa JKT pamekua ni mahali pekee nchini ambapo vijana wa makabila na dini zote wanapokutana huishi pamoja na kufanya mafunzo na kazi kama ndugu wa familia moja na hivyo kujenga umoja na mshikamano wa kitaifa.


"Awamu ya kwanza ilijenga nchi,umoja wa kitaifa, iliunda jeshi, iliandaa vijana kwa ulinzi wa nchi yao ambao walimshinda nduli Iddi Amini Dadaa, mafanikio hayo yameendelezwa na awamu zilizofuata zote .” alieleza Dkt. Stergomena


Amesema katika kulinda mipaka ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania uhuru na usalama wa nchi  Wizara kupitia JWTZ  imechangia katika kujenga uchumi imara ambapo wananchi hujishghulisha na shuguhli za uzalishaji mali bila hofu.
Aidha Serikali kupitia Wizara imeendelea kutekeleza na kuimarisha Jeshi kwa kulipatia dhana na vifaa bora na vya kisasa, rasilimali watu na nyenzo za kufanyia mazoezi ili kuwa imara wakati wote.


Mbali na hayo Dkt Stergomena amesema katika miaka 60 ya muungano ya Tanziania Sheria ya JKT Na.16 ya mwaka 1964 (The national services act no.16 1964) ilitungwa Sheria ambayo iliwezesha kuanzishwa kwa Jeshi la kujenga Taifa JKT na kuwezesha kuandikishwa vijana wa kujitolea na kwa mujibu wa Sheria
Post a Comment

0 Comments