MAANDALIZI KUELEKEA MAONYESHO MAALUMU YA WIZARA YA KILIMO BUNGENI DODOMA

 Na mwandishi wetu

Kuelekea Bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 itakayosomwa Bungeni jijini Dodoma, Mei 2 na Mei 3, 2024, Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za Kilimo zilizo chini yake wameandaa maonyesho maalumu yatakayowezesha wananchi mbalimbali wakiwemo waheshimiwa Wabunge kuweza kufahamu huduma mbalimbali zinazotolewa na Wizara hiyo kupitia taasisi zake.


Maonyesho hayo yaliyoandaliwa kwa lengo la kuongeza chachu kwa wakulima na wananchi kuelewa kwa kina dhana ya kilimo cha kisasa na huduma zinazotolewa na Wizara ya Kilimo katika kufanikisha hilo, yanatarajiwa kuanza kesho, Aprili 29, 2024 na kumalizika Mei 03, 2024 katika Viwanja vya Bunge jijini Dodoma.


Post a Comment

0 Comments