MAJIZO AJITOSA KWENYE SAKATA LA AJIRA NCHINI,AJA NA JAMBO HILI,NI MIAKA KUMI YA E.FM.

 


Na mwandishi wetu

KATIKA kuhakikisha wanawainua vijana wa kitanzania kujikwamua na tatizo la nchini kituo cha radio na tv cha E.FM na TV  wameanzisha Jukwaa lijulikanalo kama “ Kitaa Hub”likilenga kusaidia vijana kupata ajira na kujikwamua kiuchumi.   

Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho Francis Sizza maarufu kama Majizzo amebainisha hayo mapema  leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kupitia EFM atatimiza maono yake ya kuwainua vijana kupitia kampeni ya Majizzo Jobs Campaign.Majizo  amesema  Katika kutimiza miaka 10 tangua kuanzishwa kwa kituo cha redio cha E.FM ameamua kuanzisha

jukwaa la Kitaa Hub litakuwa jukwaa mahususi lenye lengo la kuwapa vijana nafasi ya kujifunza, kukua na hata kushindana katika soko la ndani na kimataifa.“ Lengo letu ni kufikia kundi kubwa la vijana kwenye field tofauti tofauti, naongelea vinyozi, fundi uashi, wapishi, wasusi, dada wa kazi, madereva, wasanii, waandishi wa nyimbo, DJS na graduates na wengine wengi Kwa kifupi ni uwanja wa kujidai onyesha uwezo wako” Amesema Majjizo.Huku naye mjumbe wa timu inayosimamia jukwaa hilo Dkt Albert Komba amesema kwamba jukwaa la Kitaa hubs litasaidia kuwajengea uwezo vijana wanaotafuta ajira na kuwaunganisha na waajiri Kwa urahisi zaidi.Aidha amesema kwa sasa kiwango Cha ajira chini kipo chini hivyo serikali na taasisi binafsi hazina budi kushirikiana kutafuta mwarobaini wa tatizo Hilo nakisusisitiza kuwa kupitia Kitaa hubs intasiadia kupunguza tatizo la ajira Kwa vijana ambao Wana vipaji vya aina mbalimbali.“Hili jukwaa la Kitaa hubs pamoja na Majizzo jobs Compaign itaweza kukutanisha vijana nchi nzima ili kuweza kuonyesha vipaji vyao,naamini kuanzishwa kwa jukwaa hili itasaidia vijana kutoa mawazo yao,bunifu zao na kuweza kufikia ndoto zao Kwa urahisi zaidi” amesema Dkt Komba.Hata hivyo vijana waliojitokeza katika mkutano huo wamepongeza kuanzishwa kwa jukwaa la Kitaa hubs kwani litawasaidia kuwasimamia katika kupata kazi nzuri na zenye staha huku wakisisitiza kuwepo Kwa usalama wa taarifa zao kwenye mtandao huo wa website.

Post a Comment

0 Comments