MAN CITY WAMEANZA MAZUNGUMZO NA WOLVES KUHUSU RAYAN AIT-NOURI

 


Manchester City wameanza mazungumzo na Wolves kuhusu uwezekano wa kumsajili winga wa Algeria Rayan Ait-Nouri, 22. (Footyball Transfer)

Tottenham wametoa ofa kwa Tosin Adarabioyo wa Fulham wakati wakijaribu kuishinda Manchester United katika mbio za kumnunua beki huyo wa Uingereza, 26. (Teamtalk).

Newcastle wanaangalia uwezekano wa kumsajili Adarabioyo pamoja na mlinzi wa kati wa Bournemouth Lloyd Kelly, 25, kwani wawili hao wa Uingereza wanamaliza kandarasi zao msimu ujao. (Telegraph – Subscription Required)

Manchester United wanaonyesha nia ya kumnunua mchezaji wa Sporting Lisbon Viktor Gyokeres lakini wanahofia kwamba Liverpool wanaweza kuharibu nafasi yao ya kumsajili mshambuliaji huyo wa Uswidi, 25. (HITC).

Post a Comment

0 Comments