MAN CITY WAONGOZA MBIO ZA KUMSAJILI MSHAMBULIAJI WA BAYERN MUNICH JAMAL MUSIALA

 


Manchester City wanaongoza kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Bayern Munich Mjerumani Jamal Musiala, 21 - lakini Liverpool , Barcelona na Paris St-Germain wote pia wanamtaka nyota huyo . (Independent)

Brentford wanatarajia mshambuliaji wa Uingereza Ivan Toney kuondoka katika klabu hiyo msimu wa joto, lakini The Bees watadai pauni milioni 50, huku Manchester United wakiwa miongoni mwa vilabu kadhaa vya Premier League vinavyomfuatilia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28.(HITC)

Sir Jim Ratcliffe amefanya mazungumzo ya ana kwa ana na mmiliki mwenza wa Newcastle United Amanda Staveley katika kujaribu kufikia makubaliano juu ya uhamisho wa mkurugenzi wa michezo Dan Ashworth kwenda Manchester United(Times)

Hali nzuri ya mchezo wa fowadi wa Arsenal Kai Havertz, 24,imewafanya The Gunners kufikiria upya mipango yao ya uhamisho wa majira ya joto, huku kukiwa na uwezekano wa kilabu hiyo kuacha mipango ya kumnunua Toney.(Mirror)

Post a Comment

0 Comments