MASOKO YA MITAJI YAPANDA HADI TSH TRIL 40

 


Masoko ya mitaji ya Tanzania yameongezeka kwa asilimia 26 katika jumla ya thamani ya uwekezaji kutoka shilingi trilioni 33.3 iliyorekodiwa Februari 2021 hadi shilingi trilioni 40.1 mwezi Februari mwaka 2024.

Akizungumzia hatua hiyo kubwa ya masoko yenye utulivu na uthabiti unaowezeshwa na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) Tanzania, Ofisa Mtendaji Mkuu wa CMSA CPA Nicodemus Mkama amesema nchi inaendelea na mapambano licha ya athari za Covid-19 na mivutano ya kijiografia duniani.

Jitihada za serikali ya awamu ya sita katika kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji nchini, yamechagiza kupatikana kwa matokeo haya.

Thamani halisi ya miradi ya uwekezaji wa pamoja imekuwa na ongezeko kubwa la asilimia 297.1 hadi kufikia shilingi trillion 2.0 mwezi Februari ikilinganishwa na shilingi bilioni 500.3 mwezi Februari 2021.

Mafanikio haya yameiweka Tanzania katika ramani ya masoko ya mitaji ya kimataifa ambayo yanatoa bidhaa za kibunifu na endelevu zinazovutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

Post a Comment

0 Comments