MKUU WA MAJESHI KENYA AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA HELIKOPTA

 Na mwandishi wetu

 Rais wa Kenya, Dkt. William Ruto ametangaza kifo cha Mkuu wa Majeshi wa Nchi hiyo Francis Ogolla ambaye amefariki kwa ajali ya helikopta iliyoua Wanajeshi wengine 9 na kujeruhi wawili.

Ruto amesema Helikopta hiyo ilikuwa na Wanajeshi  11 akiwemo Mkuu huyo wa Majeshi ambapo waliofariki ni 9 akiwemo Rubani na Wanajeshi wawili wamenusurika. 

Helikopta hiyo ilikuwa inawasafirisha Maafisa Wakuu wa Jeshi wakitoka kukagua Shule zilizokuwa zinajengwa baada ya mashambulizi ya Majambazi katika eneo la Pokot Nchini Kenya.

Post a Comment

0 Comments