MNEC CHACHA ASISITIZA WANACCM KUWA NA UMOJA.

 
Na mwandishi wetu

Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (MNEC) Chacha Wambura (WAJA) amewataka Wana chama  wa chama cha Mapinduzi (CCM) kuendelea kushikamana na kuwa na umoja katika kuelekea Uchaguzi wa Serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.


Mnec Chacha amesema hayo mapema Leo,Wilayani Bunda wakati akiwa kwenye ziara ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara ,Abdulrahman Omari Kinana ambaye yupo Mkoani Mara kwenye ziara ambayo Lengo lake ni kukijenga Chama.


Amesema wao kama Wanaccm Wajibu wao mkubwa ni kushikamana na kuhakikisha wanapata ushindi kwenye chaguzi zilizopo mbele.


"Natambua sisi ndio chama Bora ambacho kinaongoza Nchi lakini ubora wetu utakuja zaidi ni pale tutakapoendelea kuwa wamoja na kusimama kwa masirahi mapana ya chama na kuendelea kutangaza mema ambayo Rais Wetu Samia Suluhu Hassan anayafanya kwa Taifa"Chacha Wambura Mnec.


Sanjali na haya Mnec Waja amewataka Wanawake kujitokeza kugombea nyazifa Mbalimbali pindi kwenye chaguzi za Serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025...

Post a Comment

0 Comments