MSIENDE KUTENGENEZA MIGOGORO - DKT SAMIA

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wateule kuwa sehemu ya kuwaunganisha watu na sio kutengeneza migogogoro baina ya jamii/wananchi.

Dkt Samia ametoa wito huo hiyo leo April 04, 2024 Ikulu Jijini Dare salaam wakati akiwaapisha viongozi aliowateua siku za hivi karibuni.

“Niwaombe kafanyeni kazi kwa kuwaunganisha watu,nendeni katatueni migogoro iliyoko huko mnakokwenda na msiende kutengeneza migogoro” Amesema Dkt Samia.

Aidha Mhe Rais Dkt Samia amewasisitiza viongozi hao wateule kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuleta mwanya wa kuwahudumia wananchi kwa ufanisi.
Post a Comment

0 Comments