RAIS DK.MWINYI ASHUKURU KWA DUA ZA HAYATI MZEE MWINYI

*RAIS DK.MWINYI ASHUKURU KWA DUA ZA HAYATI MZEE MWINYI*


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema familia ya Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi imefarijika sana tangu alipofariki dunia kwa Dua zilizofanyika katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya kumuombea.


Ameshukuru kwa Dua  zilizosomwa kumuombea Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi. 


Rais Dk.Mwinyi amesema hayo katika kisomo cha Dua  ya Arubaini ya   Hayati Ali Hassan Mwinyi pamoja iftari iliyofanyika viwanja vya Ikulu Mnazi Mmoja tarehe: 07 Aprili 2024.


Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amesema leo ni siku ya kipekee asubuhi imefanyika Hitma ya  kuombea Hayati Sheikh Abeid Amani Karume na  jioni Hayati Ali Hassan Mwinyi. 


Dua hiyo imehudhuriwa na  Viongozi mbalimbali wa Serikali, Vyombo vya ulinzi na usalama, Dini , Vyama vya Siasa na Wananchi.


Post a Comment

0 Comments