RC CHALAMILA ATAKA BEACH YENYE HADHI YA KIMATAIFA

 
Na mwandishi wetu

-Akerwa na mazingira ya uchafu Coco beach


-Asema Coco beach ni ya wanyonge akemea uendelezaji usio na tija katika fukwe hiyo ya Coco beach


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila katika muendelezo wa ziara yake leo April 18,2024 amatembelea fukwe ya Coco beach Wilaya ya Kinondoni Jijini humo.


Akiwa katika eneo la fukwe ya Coco RC Chalamila alipata wasaa wa kukagua na kuongea na wafanyabishara wa eneo hilo pamoja na uongozi wa Manispaa ambapo amepongeza juhudi zinazofanywa na Manispaa lakini hakufurahishwa na hali ya usafi katika fukwe hiyo.


Ambapo ameagiza uongozi wa Kinondoni kushirikiana na wafanyabishara wenye uwezo ili kugharamia uwekaji wa perving katika eneo la mbele ya mabanda ili kuwe nadhifu na maji yasituame ovyo hasa Kipindi hiki cha msimu wa mvua


Aidha RC Chalamila amewataka viongozi wa Manispaa ya Kinondoni kufikiri zaidi namna ya kuboresha fukwe hasa upande wa kuanzia police mercy, Seacliff hotel ili kuwe na hadhi ya kimataifa " Nataka tuwe na fukwe hata Rais wa nchi nyingine akitembelea DSM aweze kuletwa katika fukwe hiyo iwe ni fukwe yenye hadhi ya kimataifa" Alisema RC Chalamila


Vilevile RC Chalamila ameutaka uongozi wa Manispaa ya Kinondoni kutofanya uendelezaji ambao hauna tija kwa mfano sehemu ya fukwe ya upande wa kuelekea Daraja la Tanzanite ambako viongozi wengi wa ubalozi wanaishi kuacha mara moja asingependa kuona uendelezaji wa aina yoyote katika sehemu hiyo.


Pia RC Chalamila amesistiza kutokubali kuchukua au kupata pesa bila kuangalia uhai wa kesho vilevile amesema kila mmoja awe na mkakati wa usafi kwa kuwa balozi wa kwanza wa usafi ni mimi na wewe.


Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Saad Mtambule amekiri kupokea maelekezo kwa ajili ya utekelezaji ikiwemo suala la usafi na ubunifu katika fukwe ili kuleta tija kwa Jamii ya wanakinondoni, Mkoa na Taifa kwa ujumla.


Post a Comment

0 Comments