STAMICO KUENDELEA KUWAPA SHUGHULI ZA KIUCHUMI WATU WA MAKUNDI MAALUMU.

 


Na mwandishi wetu

Shirika la Madini la Taifa *STAMICO*, limejiwekea malengo ya kuendelea kuwasaidia watu wa makundi maalumu kama vile walemavu ili waweze kujikwamua kiuchumi kwa kuwapa shughuli za kiuchumi kama vile Uwakala wa Kusambaza wa Nishati safi ya Rafiki Briquettes na kuwapa mafunzo ya uchimbaji madini na kuwasimamia ili waweze kunufaika na Rasilimali madini zilizoko nchini.


Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO *Dkt Venance Mwasse* ameeleza hayo Tarehe 8 Aprili 2024 wakati wa Futari ya pamoja na watumishi wa *STAMICO* pamoja na watu kutoka makundi maalumu tukio lilofanyika Dodoma. Tukio hili lilihudhuriwa na viongozi wa kidini, akiwepo Mwakilishi wa Sheikn wa Wilaya, Sheikn Abdurahman Issa pamoja na Katibu Sheikn Shafii Husein Ramadhan.


“Hii sio mara ya kwanza kwa sisi kufuturisha watu wa makundi maalumu kipindi hiki cha mwezi Mtukufu tayari tumefanya hivyi katika Mkoa wa Lindi kabla ya kufanya tukio hili  leo Jijini Dodoma na hatuishii tu kuwapa chakula bali tunawapa mafunzo, na fursa za kiuchumi kama vile uwakala wa usambazaji wa nishati safi, kuwajengea uwezo wa kushiriki kwenye shughuli za Madini kwa kuwapa mafunzo na kuwasimamia ili nao waweze kunufaika na Rasilimali hizi za Madini”, alisema Dkt Mwasse.


Aidha *Dkt. Mwasse* ameeleza kuwa tayari STAMICO wamewawezesha wenye usikivu hafifu mkoa wa Geita kupata mafunzo ya uchimbaji Madini na kuwapa leseni ya uchimbaji Madini ya Dhahabu na kwa sasa wanachimba Dhahabu katika mgodi uliopo Masumbwe, Geita, na Shirika linaendelea kuwasimimamia ili waweze kunufaika na Rasilimali hiyo ya Madini. 


Muwakilishi wa Sheikh wa Wilaya *Sheikn Abdurahman Issa* amewapongeza STAMICO na kuwaomba kuendelea na utaratibu huo kwani wanafanya jambo zuri kwa Jamii hiyo ya watu wa Makundi Maalumu na ni sambamba na matakwa ya Mwenyezi mungu.

Post a Comment

0 Comments