"TOKA NITAMKE VILE MIKOSI IMENIANDAMA"DULLA MAKABILA

 


Kufuatia Tamko la Dulla Makabila Baada ya kusema hadharani eti Ajafunga mwenzi mtukufu wa Ramadhani pia Akiwekewa mil 100 na Quran atachagua Mil 100, 


Basi leo amekiri kuwa tangu atamke maneno hayo, Mpaka sasa mambo yake yamekuwa yakienda kombo  tofauti na alivyotarajia hivyo mikosi ya rejareja ambayo inamfanya baadhi ya kazi zake za kimziki alizotakiwa kufanya kwenye kipindi hiki cha mfungo kukwama.


Leo pia ikiwa ni muendelezo wa mikosi kwenye maisha yake, kupitia ukurasa wake wa Instagram Dulla ameelezea jinsi alivyopata ajali mbili siku ya jana na leo. 


"Jana tulikuwa na show Tanga wakati tunaenda njiani tulipata ajali na alphard ikaharibika tukaiacha Tanga,  leo tena wakati tunarudi tumechukua gari nyingine kwa ajili ya kuwahi ndege ya mchana maana kesho tuna show ya mkesha wa mwenge Moshi, tumefika Bunju tumepata ajali tena"- ameandika Dulla Makabila


Post a Comment

0 Comments