TUTAHAKIKISHA MIKOPO YA ASILIMIA 10 INAWAFIKIA VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU-MHE.NDEJEMBI

 Na mwandishi wetu,Bungeni Dodoma 

WAZIRI wa Nchi,ofisi ya Waziri mkuu,kazi,vijana,Ajira na wenye Ulemavu Mheshimiwa Deogratius Ndejembi amesema ofisi hiyo itashirikiana na ofisi ya Rais TAMISEMI Katika kuwezesha vijana na wenye Ulemavu mikopo inayotolewa na Halmashauri ili wafanye shughuli zenye tija.


Mheshimiwa Ndejembi amesema hayo wakati akichangia hotuba ya Bajeti ya ofisi ya Waziri mkuu kwa mwaka wa  Fedha 2024/25 Bungeni Jijini Dodoma April 15,2024


Amelihakikishia Bunge Kuwa ofisi yake itaendelea kuratibu wizara za kisekta ili vijana wengi Nchini waweze kunafaika na fursa zinazotolewa na serikali yao Katika miradi ya Kimkakati,kilimo,madini,Mifugo na uvuvi.

 

Kwa upande mwingine Mheshimiwa Ndejembi alisema ofisi hiyo kupitia kitengo Cha huduma za Ajira (TaESA) wanaendelea na majadiliano na nchi mbalimbali ili kuona namna ya kupata fursa watanzania wengi kuajiriwa nje ya nchi.

Post a Comment

0 Comments