VIONGOZI WA YANGA WATUMIE KANUNI YA KUKATA RUFAA-MASELE

 


Na mwandishi wetu

Yanga inaweza kukata rufaa CAF kupitia kifungu cha sheria za mpira za CAF namba XVI kifungu namba 3 kupinga kitendo cha kukataliwa goli alilofunga Aziz Ki.


Masele ameshauri Viongozi wa Yanga watumie kanuni hiyo kwani kifungu hicho ni mahususi kuhusu utawala na upangaji wa matokeo ambapo iwapo ikithibitika ni kweli basi Mamelodi watanyang’anywa matokeo na kupewa Yanga SC.


“Klabu ya Yanga inaweza kukata rufaa kwa baraza linalosimamia soka na kuripoti rasmi kesi ya upangaji matokeo chini ya kifungu XVI kifungu kidogo cha 3 kinachosema;XVI. FRAUD -ADMINISTRATIVE ERROR - MATCH FIXING. Na Kama itathibitishwa basi Mamelodi inaweza kuondolewa kwenye michuano na  Yanga akapata upendeleo” 


Stephen Julius Masele - Aliyewahi kuwa Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika (PAP) na Mbunge wa Shinyanga Mjini.

Post a Comment

0 Comments