WANANCHI JIRIDHISHENI NA UHALALI WA VITUO VYA HUDUMA ZA MACHO NA MIWANI TIBA

 
Na WAF - DAR ES SALAAM 

Serikali imewataka wanachi kuchukua tahadhari ya huduma za Macho na Miwani tiba zinazo tolewa ili kuepuka madhara ambayo yanaweza kumkumba mtu ikiwepo kupoteza uoni au hata upofu.

Rai hiyo imetolewa na Baraza la Optometria Nchini Kupitia kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Mohamed Mang'una, Aprili 19,2024 jijini Dar es Salaam. 


"Nitumie fursa hii kwa wakazi wa Dar es Salaam na nchi nzima kwa ujumla kuhakikisha wanajiridhisha uhalali wa vituo na watoa huduma za tiba ya macho na miwani tiba kabla ya kupokea huduma yoyote  ili kuepuka Madhara ikiwemo vifo na  upofu wa kudumu" amesema Mang'una na kuongeza

"Jamii ijenge hulka ya kupitia mifumo rasmi ya utambuzi wa watoa huduma za optometria kupitia tovuti ya Mfumo wa Usajili wa Vituo vya afya wa Wizara ya Afya - HFRS ( hfrs.moh.go.tz)" amesisitiza Mang'una.

Amewataka wananchi, wasi sidanganyike, iwapo wana tatizo la macho, nenda kwenye vituo halali viliyosajiliwa kwa ajili ya huduma za Macho na Kioptometria (Miwani tiba).

Dkt. Mang'una ameongeza kuwa kwa Mkoa wa Dar Es Salaam huduma ya kupimwa au kupata miwani tiba inazidi kuimarika kwani  jumla ya Vituo 89 vya optometria vimesajiliwa na pia  hospitali zote za Serikali na binafsi zinatoa huduma hizi.

Kwa upande wake Msajili wa Baraza la Optometria Nchini, Sebastiano Millanzi amekemea kitendo cha watu wasio wanataaluma wa optometria kuvamia fani hiyo na kusisitiza Wataendelea ukaguzi wa kushtukiza mara kwa mara ili kuiepusha jamii na Waoptometria Vishoka.

"Vituo tulivyovifungia pia vimetozwa faini baada ya kukutwa na watoa huduma wasiokuwa na taaluma na wamili walio kinyume na sheria.

Nae Mwanasheria kutoka Wizara ya Afya, Abeli Mshashi amewakumbusha wamiliki na wale wote wenye nia ya kumiliki vituo vya kutolea huduma za Optometria kuhakikisha wafuata taratibu na sheria kwa mujibu wa sheria ya Optometria ya mwaka 2007.


Baraza lipo mbioni kuandaa stika maalumu za kutambulisha Vituo kuonyesha vituo vilivyo kidhi vigezo na vimesajiliwa. 

Post a Comment

0 Comments