WANANCHI WA KILOSA WAJUMUIKA KUFANYA MAOMBI KWA DKT SAMIA SULUHU HASSAN NA KUSHIRIKI FUTARI YA PAMOJA

 📍KILOSA, MOROGORO

Na mwandishi wetu


Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka ameungana na Viongozi wa dini wa madhehebu mbali mbali, Vyama vya Siasa, Taasisi za Serikali na Binafsi, Mashirika na wananchi mbali mbali katika maombi na ibada ya Duah na Sala kumuombea Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kisha kujumuika katika futari ya Pamoja.


Shuhuli hiyo adhimu imefanyika katika maakazi ya Mkuu wa Wilaya wa Kilosa,  imehudhuriwa na wananchi kutoka katika viunga mbali mbali vya wilaya hiyo.


" Pamoja na mvua kubwa inayonyesha nawashkuru sana wananchi kwa kujitokeza kwa wingi kila aliyesikia kuna maombi kwa Dkt Samia Suluhu Hassan ameingia njia kufika hapa, hii ni ishara ya mahaba na mapenzi makubwa mliyonayo kwa Rais wetu....


Lakini pia kitendo cha kuftari pamoja leo hii kwa mara ya kwanza nimeshuhudi umma mkubwa kama huu, Alhamdulilah riziki imetawanyika na kila mmoja imemfikia ni ishara njema ya Umoja, Mshikamano na Upendo tulionao wana Kilosa, Allahu Bariki"
Post a Comment

0 Comments