"WANAOENEZA CHUKI NI MAADAU WA TAIFA NA ADUI WA TAIFA LETU NI ADUI YETU SISI VIJANA" CDE MWAKINYA.*

 


*📌📌"WANAOENEZA CHUKI NI MAADAU WA TAIFA NA ADUI WA TAIFA LETU NI ADUI YETU SISI VIJANA" CDE MWAKINYA.*


Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Tanzania Bara Komredi Mussa Mwakitinya amesema mtu yeyote anayeeneza chuki dhini ya Serikali katika Taifa la Tanzani basi mtu huyo ni Adui wa Tanzania ni Adui wa Vijana wote nchini hivyo hawana budi kumchapa kwa hoja


"Sisi kama Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi hatuamini katika Maandamano ya kujaza Chuki kwa wananchi dhidi ya Serikali, tunaamini katika namna ya kuwezo kukaa chini kujadiliana na kuwa na hoja namna ya kufanya mambo yaende Vizuri, Sasa tunaona kuna watu wamekosa hoja kwenye Taifa la Tanzania wanakimbilia Maandamano"

 

"Tanzania tumepiga hatua kubwa sana katika  ulingo wa Demokrasia na hata maridhiano tuliyonayo sasa ambayo yamewapa Uhuru vyama vya Siasa kufanya mikutano ya hadhara hatukuingia barabarani kuandamana bali  Chama cha Mapinduzi kilikaa chini na Vyama vingine tukaridhiana mambo yakaenda sawa lakini sasa cha ajabu kuna wenzetu wamekosa hoja na kwa sababu wao lengo ni kuvuruga Amani ya nchi hii wao wameamua kuyakimbia maridhiano ya kidemokrasia wanaingiza watu Barabarani, kuingza watu barabarani inaonyesha kuwa wamekosa uvumilivu".


Aidha Komredi  Mwakitinya amesema wapo watu wao wamekosa uvumilivu na kukimbilia maandano lakini pia katika Maandamano yao kazi yao kubwa ni kujaza Chuki kwa wananchi Jambo ambalo sio sahihi na linahatarisha Amani ya Taifa letu hivyo wanapaswa kupingwa kwa namna zote kwani hawa ni maadui wa Taifa letu.


"Hawa watu wanaoandamana wanajaza chuki kwa watanzania kitu ambacho sio sahihi, tunoana wanataka kuvuruga Amani katika Taifa letu la Tanzania na sisi mtu anayetaka kuvuruga Amani yetu huyu ni adui wa Taifa na sisi Vijana Adau wa Taifa ni Adaui yetu hivyo lazima tumchape kwa hoja. Ndugu


Komredi Mwakitinya amesema Amani ya Tanzania ni kitu kikubwa kuliko kitu chochote kile hivyo UVCCM haipo tayari kuona Amani ya nchi hii inapotea kwani wameona mataifa mengine yaliyoharibu  Amani  yao wananchi wake wanavyoteseka.============

Post a Comment

0 Comments