WAZIRI JAFO AMESHIRIKI HALFA FUPI YA KUWAAGA WATENDAJI WASTAFU KUTOKA NEMC

 


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ameshiriki hafla fupi ya kuwaaga watendaji wastafu kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) iliyofanyika usiku wa tarehe 27 Aprili, 2024 jijini Dar es Salaam.

 

Miongoni mwa wastaafu walioagwa ni Dkt.Samuel Gwamaka aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu NEMC, Bw.Lewis Nzali aliyekuwa Meneja wa Kanda ya Kaskazini na Bw. Anold Kisiraga. 

 

Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na viongozi na watendaji kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na NEMC wakiwemo Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Bi. Christina Mndeme, Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi NEMC Prof. Esnat Chaggu, Mkurugenzi Mkuu NEMC Dkt. Immaculate Semesi na Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Kemilembe Mutasa.

 

Katika hafla hiyo pia, NEMC iliwaaga watumishi wa Idara ya Fedha waliopata fursa ya kulitumikia Taifa nje ya Baraza ambao ni Mhasibu Mkuu Bi. Esther Subi na Mkurugenzi wa Utawala Bw. Charles Wangwe
Post a Comment

0 Comments