WAZIRI NDEJEMBI AONGOZA UJUMBE YA MKOA WA ARUSHA NA TUCTA KUKAGUA UWANJA WA SHEKHE ABEID ARUSHA

 


Na mwandishi wetu

WAZIRI wa Nchi,ofisi ya Waziri mkuu kazi,vijana,Ajira na watu wenye Ulemavu Mheshimiwa Deogratius Ndejembi amekutana na kufanya kikao cha pamoja na shirikisho la Vyama vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) lengo likiwa ni kujadili maandalizi ya maadhimisho ya Sherehe za Mei mosi zitakazofanyika Jijini Arusha mei mwaka huu.


Katika Hatua nyingine Mheshimiwa ameuongoza ujumbe wa Mkoa wa Arusha na  TUCTA kukagua uwanja wa shekhe Abeid Karume Jijini Arusha ambapo wamebaini maeneo ya maboresho ya uwanja huo utakaotumika kwenye maadhimisho.


Katika Ziara hiyo ameshiriki kamishna wa kazi-ofisi ya Waziri mkuu -kazi,vijana,Ajira na watu wenye Ulemavu Suzan Mkungwa ,katibu tawala Mkoa Arusha Ndugu Missaile Mussa ,viongozi wa Vyama vya wafanyakazi wakiongozwa na Rais wa TUCTA Tumaini Nyamhokya ,wakuu wa wilaya za Mkoa WA Arusha pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri zake.
Post a Comment

0 Comments