ZANZIBAR KUDUMISHA USHIRIKIANO NA OMAN

 


Na mwandishi wetu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj. Dk. Hussein Ali Mwinyi ameahidi kuendeleza ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya Zanzibar na Oman. 


Rais Alhaj Dk.Mwinyi amesema hayo leo katika hafla ya  futari iliyoandaliwa na  Balozi Mdogo wa Oman Zanzibar,  Mhe.Said Salim Al Sinaw iliyofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip, Uwanja wa ndege Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe: 04 Aprili 2024.


Kwa upande mwingine Rais Dk. Mwinyi amesema Serikali ya Oman imeendelea kuwa mstari wa mbele katika kuisaidia Zanzibar katika miradi ya Maendeleo ikiwemo ukarabati wa majengo ya kihistoria, Afya na Elimu.


Post a Comment

0 Comments