ASKOFU MALASUSA AGUSIA MMONYOKO WA MAADILI,AZINDUA SHULE HII.

 


Na mwandishi wetu

MKUU wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Askofu Alex Malasusa ,amesema ili tuwe na jamii njema wazazi wametakiwa kuanza kuwalea watoto kimaadili wakiwa msingi ili kusaidia kuondokana na tatizo la mmonyoko wa maadili kwenye jamii.


Askofu Malasusa ameyasema hayo leo mapema jijini Dar es Salaam wakati Uzinduzi wa shule ya msingi na awali ya Jerusalem Mbezi Beach .


"Ili tume na jamii yenye maadili mema ni lazima maadili yajengwe yakiwa msingi,maadili hayatokei tu"Amesema Askofu Malasusa.


Hata hivyo,Kiongozi huyo wa kiroho pia amewata wazazi,walimu na viongozi wa kidini kuungana na kupambana na vitu vinavyochochea mmonyoko wa maadili.


"Maadili hayatokei tu,au huwezi kwenda kununua maadili ni lazima tushirikiane,mimi,wewe tuungane κwenye kurudisha maadili mema kwenye jamii yetu"ameongeza kusema.


Akizungumzia shule hiyo ya Jerusalem,Askofu Malasusa, amesema maazimio ya kuanzishwa shule hiyo yametokana mkutano mkuu wa Dayosisi uliketi hivi karibu kuanza kuweka mkazo kwenye elimu,tulianza ngazi ya sekondari sasa tupo kwenye msingi.


Askofu Malasusa,amesema shule hiyo ni yakipekee na kuwataka wazazi kuwaleta watoto shuleni hapo.


"Shule hii ni ya watu wote ,shule hii haina ubaguzi na hatutambagua mtu kwa rangi,dini kila mtu atapata elimu,kwani Yesu hakuja duniani kwa ajili ya watu flani alikuwa kwa watu wote"


Kwa Upande wake Mratibu wa Elimu wa Dayosisi ngazi ya pwani,Agnes Lema,amesema shule hiyo itakuwa ikitumia mtaala wa elimu ya dini kwa ajili ya kuwaleta watoto kwa maadili mema.


Lema amesema sababu ya kuanzisha shule ya Jerusalem baada ya kubaini kuwepo na tatizo la mmonyoko wa maadili kwenye jamii.


"Tumeona bado kuna changamoto ya kukosa kwa maadili kwa watoto na jamii kwa ujumla,hivyo hapa tutasaidia kumlea mtoto maadili mema"

Post a Comment

0 Comments