BAJETI YA WIZARA YA MAJI

 


#BungeniLeo


🗓️Alhamisi 09 Mei, 2024.


*BAJETI YA WIZARA YA MAJI*


Nimepata nafasi ya kuchangia kwenye BAJETI ya Wizara ya Maji iliyowasilishwa leo na Waziri Mwenye dhamana Mhe. Jumaa Awesso (Mb.).

Ni wizara ambayo imesababisha Jimbo la Muhambwe kupokea Jumla ya Kiasi Cha Tsh. Bilioni 8.5 kwa ajili ya kuboresha na kujenga miundombinu ya Maji ili kutatua changamoto za upatikanaji wa Maji jimboni kwa kuhakikisha upatikanaji wa Maji unakua Kwa kasi kutoka 54% hadi 77% (Vijijini) na 37% hadi 67% (Mjini).


Nimeiomba Serikali iingize Mto Malagarasi katika Gridi ya Taifa ya vyanzo vya Maji safi ili utumike kuwahudumia wananchi wanaoishi katika kata ya Busunzu ambayo ipo Kilomita 8 tu kutoka Mtoni ili kutatua changamoto ya upatikanaji wa Maji safi Kwa Wananchi wa Nyarulanga, Busunzu, na sehemu nyingine zote za Wilaya ya Kibondo zinazounguka Mto.


Aidha, nimeongeza kwa kuiomba Serikali kuharakisha upatikanaji wa fedha kiasi Cha Tsh. Bilioni 4.5 ili zitumike kujenga tenki kubwa zaidi la Maji juu ya Mlima Muyaga (Kitahana) litakalotumika kuvuna Maji kutoka kwenye Kisima kirefu Cha Maji cha Rusohoko ambacho huzalisha lita 350,000 za Maji kwa saa badala ya kuendelea kuhangaika na Mto Nduta. Hii itaenda sambamba na mradi wa Maji wa Nyamkokoma, Kasana na Kigina ambayo fedha yake bado haijapokelewa Jimboni ili kurahisisha Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ifikapo 2025.


#KibondoYetuTutaijengaWenyewe

#UchaguziSerikalizaMitaa2024

👇👇👇👇

https://www.instagram.com/p/C6wt92gtlXM/?igsh=MWlqMzlyaGlxb2ZwZw==

Post a Comment

0 Comments