BRIGEDIA JENERALI NDAGALA AKAGUA ENEO LILILOATHIRIKA NA MAJI WILAYA YA KIGAMBONI JIJINI DAR ES SALAAM.

 


Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya Maafa  Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu ) Brigedia Jenerali Hosea (wa kwanza kushoto) pamoja na waratibu wa Maafa Mkoa wa Dar es Salaam Ndg. Gerlad Sondo (mwenye suti) wakikagua maeneo hayo yaliozingirwa na Maji katika eneo la Mtaa wa Maweni Bondeni


Na Mwandishi wetu.Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Brigedia Jenerali Hosea Ndagala tarehe  9 Mei, 2024  amefanya ziara ya kutembelea Wilaya ya Kigamboni kata ya Mjimwema Mtaa wa Maweni kwa lengo la kuangalia madhara yaliyotokea  kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha Jijini Dar es Salaam.Awali akiwa katika kikao cha pamoja na Katibu Tawala Msaidizi (Mipango na Uratibu) Ndg. Chillah Moses katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwaajili ya kupata taarifa kuhusu hali halisi ya madhara ya mvua hizo kwa Wilaya ya Kigamboni alielezwa kuwa maeneo yaliyoathiriwa ni pamoja na Mtaa wa Maweni eneo la Bondeni  kata ya Mji Mwema pamoja na Maweni eneo la Biasi  ambayo yamezingirwa na maji  ya mvua zinazoendelea kunyesha Katika Mkoa huo.
Aidha Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu itaendelea kuratibu masuala ya menejimenti ya maafa nchini ili kuhakikisha jamii inaendelea kuwa salama na stahimilivu dhidi ya maafa.Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya Maafa  Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu ) Brigedia Jenerali Hosea Ndagala akizungumza na katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu kabla ya kuanza ziara yake ya kukagua maeneo yaliyoathirika na maji ya mvua zinazoendelea kunyesha Jijini Dar es Salaam kushoto kwake ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya menejimenti ya  Maafa sehemu ya Operesheni , Luteni Kanali Selestine Masalamado.Katibu Tawala Msaidizi (Mipango na Uratibu) Ndg. Chillah Moses akitoa maelezo juu ya eneo la Mtaa wa Maweni kata ya Mji Mwema  ambalo limezingirwa na maji yaliyotokana na Mvua zinazoendelea kunyesha katika Jiji la Dar es Salaam.

Baadhi ya Nyumba zilizozingirwa na Maji katika eneo la Mtaa wa Maweni Bondeni kata ya Mji Mwema Wilaya ya

Kigambini mkoa wa Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)


Post a Comment

0 Comments