MAENDELEO BENK YAWANEEMESHA WAMACHINGA,YAWAPA MKOPO HUU,RAIS SAMIA ATAJWA.

 


Na mwandishi wetuKATIKA kuhakikisha wanawainua wafanyabiashara wadogodogo chini benk inayofanya vizuri kwa sasa nchini,Maendeleo Benki,imesaini Mkataba na viongozi wa Kariakoo Wamachinga Association (KAWASSO) na Mmiliki wa eneo katika kijiji Magoza Mkoani Pwani kwa ajili ya kuwawezesha wamachinga wa Mkoa wa Dar es Salaam kupata viwanja vya bei nafuu isiyozidi milioni moja.


Hatua ya Benk hiyo inaendana na falsafa ya Serikali ya awamu ya sita ya kuwainua wafanyabiashara wadogowadogo nchini kuweza kujikwamua kiuchumi na kuweza kukopesheka.Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 7, 2024 jijini Dar es Salaam wakati wa kusaini mkataba wa mara ya kwanza kwa ajili ya kununua Viwanja katika eneo lililopo Mkuranga Mkoani pwani (Machinga Plot Finance), Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Benki, Dkt. Ibrahim Mwangalaba, amesema kuwa lengo la benki kuwasaidia wafanyabiashara wadogo kumiliki viwanja pamoja na nyumba.


Hata hivyo,Dkt. Mwangalaba, amesema kuwa hatua hiyo imekuja baada ya benki kupokea maombi kutoka kwa KAWASSO kuhusu kuwakopesha kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa nyumba za makazi kwa wamachinga ambapo wamekubaliana kuanza kununua viwanja vya Wamachinga 500 wa Dar es Salaam ili waweze kumiliki ardhi na hatimaye kupata makazi ya kuishi.


“Wamachinga watapa viwanja vya bei nafuu isiyozidi shilingi milioni moja kwa kila kiwanja, huku wakirejesha kidogo kidogo kwa muda wa miezi miwili, awamu ya pili tutaaza kutoa mikopo ya ujenzi wa makazi bora kwa hawa wanufaika kupitia mkopo wa nyumba (Housing Microfinance Loans)” amesema Dkt. Mwangalaba.


Dkt. Mwangalaba amefafanua kuwa umoja huo tayari wameshapa umeshapata hekari 89 katika kijiji cha Magonza Kilichopo Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani, hivyo kutokana na Changamoto inayowakabiri Wamachinga kutokuwa na dhamana zinazowawezesha kupata mikopo kupitia taasisi za fedha Maendeleo Bank imeona na kuitatua changamoto hiyo.


“Kupitia Mpango huu benki itatoa mkopo wenye thamani ya shilingi Milioni 500 kwa Wamachinga wa Kariakoo kwa awamu ya kwanza ya Mradi ili kuwezeaha kumiliki Viwanja, hivyo pesa hizo ni kwaajili ya ununuzi wa Ardhi, Usafishaji wa eneo husika, Upimaji wa Viwanja pamoja na urasimishaji ili kuwezesha mgawanyo wa viwanja kwa wanachama binafsi ili kila mnufaika aweze kuwa na hati miliki ya kiwanja Chake.” amesema Dkt. Mwangalaba.


Dkt. Mwangalaba amesema kuwa kwa awamu ya pili kwa kushirikiana na KAWASSO na umoja wa Machinga Dar es Salaam, Maendeleo Bank itatoa mkopo wa Nyumba wenye masharti nafuu na gharama ndogo ili kuwezesha Wamachinga kumiliki nyumba ya ndogo yake.


Ameeleza kuwa mpango huo utakapokamilika utawawezesha Wamachinga kumiliki ardhi na Makazi bora pia kutawaongezea sifa ya kukopesheka zaidi ili kukuza mitaji ya biashara zao na kuondoa kikwazo cha cha kutokukopesheka kwenye taasisi za fedha.


Mwenyekiti wa Machinga Mkoa wa Dar es salaam Namoto Yusufu Namoto ameishukuru Maendeleo Benki kwa kuwashika mkono na kuwasaidia kwa kuwapa mikopo ambao utawasaidia kumiliki viwanja pamoja na makazi bora

Post a Comment

0 Comments