MAMIA YA WANANCHI KUTOKA CHINA WAJITOKEZA KATIKA MAONESHO YA UTALII BEIJING CHINA
Na mwandishi wetu


 Mamia ya wananchi kutoka China walivyojitokeza kujionea Maonesho ya Utalii kabla ya Maadhimisho ya Miaka 60 ya Kidiplomasia kati ya Tanzania na China yaliyoenda sambamba na uzinduzi wa mwaka wa Utalii na Utamaduni 2024 pamoja na filamu ya "Amazing Tanzania " jijini Beijing China.


Uzinduzi huo ulifanyika usiku wa jana Mei 15, 2024 katika Ukumbi wa Taifa wa Opera na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Angellah Kairuki(Mb), Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, Waziri wa Vijana,Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe. Tabia Maulid Mwita, Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, wajumbe wa Kamati ya Rais ya Kuitangaza Tanzania akiwemo Katibu Mkuu, Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Fatma Mabrouk, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Anderson Mutatembwa, pamoja na maafisa wa taasisi mbalimbali za sekta za umma na binafsi.
Post a Comment

0 Comments