MWENYEKITI KAWAIDA AKUTANA NA WAJUMBE WA BODI VIJANA JAZZ

 

🗒️ 14 Mei, 2024

📍Vijana Social Hall-Kinondoni 


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Komredi Mohammed Ali Kawaida (MCC) amekutana Kufanya mazungumzo na Wajumbe wa Bodi ya Uendeshaji ya Bendi ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (Vijana Jazz) tarehe 14 Mei, 2024 Vijana Social Hall Kinondoni.


 Ndugu Kawaida amesema Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi chini ya Uongozi wake una dhamira ya dhati kuendeleza mambo yote Mazuri yaliyoachwa na Uongozi uliopita ikiwemo Bendi ya Vijana Jazz.


"Ilikua ni adhma yangu baada ya Uchaguzi kuhakikisha tunaendeleza yote Mazuri yaliyoachwa na watangulizi wetu, kuendeleza Jambo nzuri sio dhambi lakini kuliua Jambo nzuri ndio dhambi na Mimi sitaruhusu kuona Bendi ya Vijana Jazz haifanyi Vizuri" 


"Tuliridhia kupitia Kamati ya Utekelezaji ya Baraza kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi kuhakikisha tunaunda Uongozi wa watu wenye taaluma na uzoefu wa nziki Ili kuendesha Vijana Jazz lakini pia kutushauri namna bora tunaweza kuiendesha bendi yetu lakini pia kuwawezesha Vijana wetu kujitengenezea kipato chao ndio Maana mkapatikana ninyi" Alisema Komredi Kawaida.

#KulindaNaKujengaUjamaa

#SisiNaMamaMleziWaWana

#Kaziiendelee


Imetolewa na;

Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM-Taifa

Post a Comment

0 Comments