NAIBU WAZIRI NISHATI ASHIRIKI MKUTANO WA NISHATI SAFI UFARANSA

 


Na mwandishi wetu

Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga Leo, 14/05/2024, anashiriki Mkutano wa Nishati Safi ya kupikia ambapo Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ni mwenyekiti mwenza wa mkutano mkubwa wa Nishati Safi ya Kupikia kwa Afrika yaani Summit of  Clean Cooking in Africa unaofanyika Paris, Ufaransa. 


Mkutano huu umewaleta pamoja wadau mbalimbali wa Nishati Safi ya Kupikia Duniani, kumuunga mkono Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ameishikilia agenda hii kama Champion namba moja kwa Nishati ya Kupikia Afrika.


 Mhe. Rais, ndiye kinara wa Nishati Safi ya Kupikia Afrika na amefanikisha kuungwa mkono kwa kiasi kikubwa na wadau wa kimtaifa katika Program hii muhimu yenye manufaa kwa Tanzania, Afrika na Dunia kwa ujumla. 


Katika mkutano huu wenyeviti wenza wengine ni Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dr. Akinwumi_adesina, Mkurugenzi Mkuu wa International Energy Agency (IEA) Fatih Birol na Waziri Mkuu wa Norway Jonas Gahr Støre.


Post a Comment

0 Comments