ONGEZEKO LA MATATIZO LA AFYA YA AKILILAIBUA SHIRIKA LA AAPH ,WATAJA VYAZO VYAKE

  Na mwandishi wetu


IMEELEZWA kuwa Changamoto ya mfumo wa maisha,matumizi ya madawa ya kulevya,msongo wa mawazo pamoja na kuongezeka kwa vitendo vya Unyapaaji kwa watu mbalimbali kumechangia kuongezeka kwa matatizo ya Afya ya Akili hasa kwa Vijana.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam,Dkt Innocent Yusufu,Mtafiti Mwandamizi wa Pogram ya Being Mental Health Initiative kutoka Shirika lisilo la Kiserikali nchini,Africa academy for Puplic Helth AAPH wakati wa uzinduzi wa mradi huo.

Dkt Yusufu,amesema katika utafiti huo katika zaidi nchi 16 kutoka Bara la Afrika na maeneo mengi Duniani imeonesha kuongeza kwa vijana kati ya miaka 10 mpaka 24 wakiwa na matatizo Akili.

"Tumebaini mambo kadhaa yanayoweza kuchochea changamoto za Afya ya Akili Ugumu wa Maisha,utumiaji wa madawa ya kulevya,kutengwa kwa watu wenye matatizo mbalimbali na kupelekea watu kujiua."Amesema Dkt Yusufu.

Aidha,Dkt Yusufu,amesema katika mradi huo wamebaini pia kuwepo kwa Unyanyapaa kuhusu afya ya Akili hapa nchini kutokana na Imani za Kiutamaduni kutokana na imani za kiutamaduni,uelewa mdogo katika Jamii,na upatikanaji mdogo wa huduma za afya ya akili.

Kwa Upande wake,Dkt Mary Mwanyika Sando,Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa APPH,amewataka wazazi na walezi wa watoto kuzidisha umakini kwa watoto ili kujiepusha wa watoto wasikumbane na matatizo ya Akili.

Dkt Sando,amesema nia ya Wazazi kuwa karibu na watoto ili kuhakikisha wanapambana na dalili za mwanzo ambazo wazazi wanaweza kuzizuia kwa mtoto wenye changomoto ya ugonjwa wa Akili.

Huku Naye,Paul Sarea ,ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Afya Akili Mirembe,amesema kwa sasa bado wazazi wanashindwa kupambana na Dalili za awali za watu wenye matatizo ya magonjwa ya akili na kupelekea kuwapeleka wagonjwa kwenye hali ya juu.

Post a Comment

0 Comments