RAIS DK.MWINYI AKUTANA NA WAPCOS YA INDIA

 


Na mwandishi wetu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na RK Agrawal Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya ushauri  WAPCOS Ltd kutoka Serikali ya  India na ujumbe wake waliofika Ikulu Zanzibar tarehe: 07 Mei 2024.


 Rais Dk.Mwinyi amesema Zanzibar inahitaji miradi mingi ya uwekezaji katika sekta ya maji na umeme. 


Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi ameishukuru Serikali ya India kwa kuisaidia Zanzibar katika miradi ya maji.


Naye Mkurugenzi RK Agrawal amesema wako tayari kuendelea kushirikiana na Serikali katika miradi hiyo.
Post a Comment

0 Comments