RC CHALAMILA AKABIDHI MWENGE WA UHURU KUSINI PEMBANa mwandishi wetu

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo *Mei 13, 2024* amekabidhi Mwenge wa Uhuru 2024 Mkoa wa kusini Pemba-Zanzibar

Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Dar es Salaam ulipokelewa *Mei 8, 2024* ukitokea Mkoa wa Pwani ambapo Mkoa wa Dar es Salaam umekimbiza Mwenge wa Uhuru katika umbali wa *KM 427.78* kwa kupitia miradi *39* yenye thamani ya *Tsh 479,649,649,667* miradi ambayo baadhi ilikuwa imekamilika, na mingine katika hatua za utekelezaji

Aidha katika Wilaya zote tano za Mkoa huo Mbio za Mwenge wa Uhuru, zimetembelea, zimekagua, kuweka jiwe la msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo *miradi yote imepitishwa na Mwenge wa Uhuru 2024 hakuna mradi uliokataliwa*

Vile vile Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Mkoa huo zimeelimisha na kuhamasisha wananchi kupitia Ujumbe wa " Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu"

Pia Ujumbe wa kudumu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kuhusu mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI, Malaria, Dawa za Kulevya, Lishe na Rushwa

Sanjari na hilo Wilaya ya Ubungo ndio imehitimisha mzunguko wa Mwenge wa Uhuru katika Mkoa huo ambapo Mhe Albert Chalamila alikabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Hassan Bomboko katika viwanja vya Barafu mburahati mapema leo

 

Post a Comment

0 Comments