"SERIKALI INAENDELEA NA UTARATIBU WAKE WA KUTOA MIKOPO YA 10% KUPITIA HALMASHAURI"WAZIRI NDEJEMBI

 


Na mwandishi wetu.

WAZIRI wa Nchi ofisi ya Waziri mkuu -Kazi,vijana,Ajira na wenye Ulemavu Mheshimiwa Deogratius Ndejembi amesema Serikali inaendelea na utaratibu wake wa Kutoa mikopo ya asilimia kumi kupitia halmashauri pamoja na mikopo ya vijana kupitia mfuko wa vijana unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri mkuu-Kazi,vijana,Ajira na wenye Ulemavu .


Mheshimiwa ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni ya NMB JIWEKEE Jijini Dar es salaam.

Mheshimiwa Ndejembi amesema ipo mikakati ambayo Serikali imeendelea kufanya ili kuongeza kipato kwa Wananchi wake ikiwa ni pamoja na Kutoa mafunzo mbalimbali yanayoratibiwa na wizara kupitia Vyuo vya ufundi stadi VETA ili Kuwapa ujuzi utakaowawezesha kujiajiri.


"Serikali inaendelea Kutoa wito kwa taasisi za kifedha kuendelea Kutoa elimu kwa Wananchi hasa vijana ili kuwa na utamadani wa kujiwekea akiba itakayowasadia Mbeleni.Niwapongeza Benki ya NMB kwa kuja na wazo la NMB JIWEKEE ambalo linawagusa Wananchi   wote walio nnje ya mfumo rasmi wa Ajira ili kujiwekea akiba "Amesema Mheshimiwa Deogratius Ndejembi


Post a Comment

0 Comments