TADB YAWAJENGEA UWEZO MAAFISA MIKOPO KUTOKA TAASISI ZA KIFEDHA

 BENKI ya Maendeleo ya kilimo (TADB)wametoa mafunzo kwa Maafisa mikopo na wataalam wa kilimo Nchini ikiwa na lengo la kuweza Kutoa huduma mikopo Katika sekta ya kilimo,TADB imeandaa mafunzo haya kwa kushirikiana na Benki  kuu ya Tanzania (BoT) na Taasisi mbalimbali za  kifedha,Mafanzo  hayo yamefanyika Leo Ijumaa Mei 03,2024 Katika ukumbi wa Benki kuu Posta Jijini Dar es salaam.


Akizungumza na waandishi wa Habari Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya kilimo(TADB)Dkt Kanaely Nnkano amesema Kuwa Dhumuni la Kutoa mafunzo hayo ni kuweza kwenda Kutoa mikopo kwenye sekta nzima ya kilimo kwani Tumekuja na wahitimu takribani 52 kutoka Katika kwenye Benki ushirika 20 ambazo zimeshiriki mafunzo haya.

"Tumeamua Kutoa mafunzo haya hadi mikoani kote kutokana na wakulima waweze kupata uelewa kuhusu kilimo kimekuwa kikiendesha mafunzo kama haya hivyo mpaka sasa mfuko wetu wa guarantii umeweza kudhamini mikopo 270 na mikopo hiyo imetolewa na Benki la shirikahilo na pia walengwa wa kilimo wa moja kwa moja tumewafikia takribani  watu 24,000"amesema Dkt Kanaely Nnkano


Kwa upande wake makamu mkuu wa chuo kutoka chuo Cha Benki ya Tanzania mkoani Mwanza Ephurem Masanguti amesema"Sisi ni sehemu ya Benki kuu tukiwa na majukumu makubwa ya kuweza kuelemisha Umma ikiwa pamoja na mabenki,wafanyakazi wa benki kuu na wanataalum wa taalum mbalimbali Katika Kutimiza majukumu yetu Benki kuu ya Tanzania inaelemisha Umma na kuchangia dira" 

Post a Comment

0 Comments