TRILIONI 1.24 ZA WIZARA YA KILIMO KUBADILI SURA YA SEKTA YA KILIMO TANZANIA

 


Na mwandishi wetu

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeidhinisha matumizi ya  ya Shilingi trilioni 1.24 kwa ajili ya Wizara ya Kilimo katika mwaka 2024/2025 kwa ajili ya  utekelezaji   wa mipango mbalimbali iliyoainishwa ili kuendelea kukuza Sekta ya Kilimo nchini.

Kwa mujibu wa Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) amesema Wizara imeongeza kipaumbele kimoja na hivyo kufanya vipaumbele vya mwaka 2024/2025 kuwa sita (6) vitakavyotekelezwa kupitia mikakati 27.

Vipumbele hivyo ni pamoja na kuongeza tija na uzalishaji (Increase Productivity and Production), kuongeza ajira zenye staha na ushiriki wa vijana na wanawake kwenye kilimo,kuimarisha usalama wa chakula na lishe, kuimarisha upatikanaji wa masoko, mitaji na mauzo ya mazao nje ya nchi, kuimarisha Maendeleo ya Ushirika pamoja na kuimarisha Matumizi ya Mifumo ya TEHAMA katika Uendelezaji wa Sekta ya Kilimo.

Post a Comment

0 Comments