TUENDELEE KUIOMBEA NCHI NA VIONGOZI WAKE-DK.MWINYI

 Na mwandishi wetu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi amewaomba Waumini wa Dini ya Kiislamu kuendelea kuwaombea Dua Viongozi ili watimize majukumu yao na  kutekeleza ahadi walizoahidi.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika sala ya Ijumaa Msikiti wa Qubaa Mbweni Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 10 Mei 2024.

Pia Rais Dk.Mwinyi amewatembelea Wazee akiwemo  Mbunge wa zamani Jimbo la Amani ,  Mzee Hassan Rajab nyumbani kwake Kisauni na Mjumbe wa  Baraza la Wazee  CCM Kisiwandui, Bi Maryam Hengwa nyumbani kwake kwa Mchina Mkoa wa Mjini Magharibi.
Post a Comment

0 Comments