UREJESHAJI WA MAWASILIANO BARABARA YA DAR - LINDI UNAENDELEA USIKU NA MCHANA

 Na mwandishi wetu

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akikagua kazi ya urejeshaji mawasiliano ya barabara ya Lindi – Dar es Salaam ambayo inaendelea kufanyika usiku na mchana ili kuhakikisha huduma za usafiri na na usafirijishaji zinarejea ifikapo siku ya Alhamisi.


Waziri Bashungwa akiwa amesalia katika Mkoa wa Lindi ili kusimamia timu ya wataalamu wa Wakala ya Barabara (TANROADS) na makandarasi huku akisisitiza kuwa kazi itafanyika usiku na mchana ili kuhakikisha zoezi hilo linakamilika ndani ya saa 72 alizoeleza awali.


Aidha, Waziri Bashungwa amemuagiza Mtendaji Mkuu wa TANROADS kuimarisha kitengo cha dharura ili kuwa tayari kukabiliana na changamoto yoyote itakayojitokeza ambayo inaathiri miundombinu ya barabara na Madaraja.

Post a Comment

0 Comments