VIJANA ELFU 20 WANUFAIKA NA UTEKELEZAJI WA PROGRAMU YA KUJITOLEA-WAZIRI NDEJEMBI

 


Na mwandishi wetu,Dar es salaam

WAZIRI wa Nchi ofisi ya Waziri mkuu-Kazi,Vijana,Ajira na wenye Ulemavu Mheshimiwa Deogratius Ndejembi amesema kwa  kipindi cha miaka mitatu zaidi ya vijana 20,000 walishiriki programu ya kujitolea "internship" ambayo iko chini ya ofisi ya Waziri mkuu ambapo kati ya vijana 3,773 walipata Ajira serikalini na sekta binafsi.


Mheshimiwa Ndejembi ameyasema hayo Leo Jijini Dar es salaam Katika halfa ya ugawaji tuzo za mashindano ya TEHAMA kwa Wanafunzi wa vyuo vikuu Nchini.

Amesema Mpango wa Serikali ya awamu ya sita ni kuhakikisha kuwa inaboresha mazingira kwa vijana kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuongeza idadi ya vijana wenye ujuzi na utaalam wanaoajiriwa serikalini na sekta binafsi.


"Ofisi ya Waziri mkuu itaendelea kusimamia 'internship' kwa vijana wetu lakini pia kuboresha mazingira ya vijana hao wanapomaliza waweze kupata Ajira iwe Serikalini au sekta ya binafsi na kuwezesha pia kupata Ajira ndani na nje ya nchi"alisema Mheshimiwa Deogratius Ndejembi
Post a Comment

0 Comments