WABUNGE WAPATA ELIMU SEKTA YA UMEME NA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

 



Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo Aprili 30, 2024 bungeni jijini Dodoma ameshiriki katika Semina ya Wabunge  iliyoandaliwa na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati za  REA, TANESCO na TPDC ya kuwajengea uwezo wabunge kutokana na maswali mbalimbali waliyouliza kipindi cha Maonesho ya Wiki ya Nishati yaliyofanyika katika Vwanja vya Bunge Jijini Dodoma


Mada zilizowasilishwa ni kukatika kwa umeme na hatua zitakazochukuliwa pamoja na  Nishati Safi ya Kupikia ambapo Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Mhe . Mussa  Zungu (Mb) alifungua semina hiyo. 


Semina hiyo imehudhuriwa pia  na Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Judith Kapinga, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba na Watendaji mbalimbali Wizara ya Nishati.










Post a Comment

0 Comments