WAZIRI MKUU MAJALIWA AMEWASILI SONGWE,KUSHIRIKI MBEYA TULIA MARATHON 2024

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Mei 10, 2024 amewasili uwanja wa ndege wa Songwe ambapo kesho Mei 11, 2024 atakuwa mgeni rasmi katika mbio za Mbeya Tulia Marathon 2024.


Akiwa mkoani Mbeya, Waziri Mkuu atakagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi.


Pichani, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera, Viongozi wa vyama vya siasa na Serikali, viongozi wa dini na mila.

Post a Comment

0 Comments