ZIMAMOTO WAZINDUA NYUMBA ZA MAKAAZI NA MAGARI.


Na mwandishi wetu


DODOMA.

Mei 13, 2024

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.Mhandisi Hamad Masauni (Mb) amezindua Nyumba za Makaazi ya Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji zilizopo Kikombo Jijini Dodoma. 

Uzinduzi huo umefanyika sambamba na  uzinduzi wa Magari 12 ya kuzimamoto,  yakiwemo Magari mawili ya Ngazi yenye uwezo wa kufanya maokozi katika Majengo Marefu yenye urefu wa ghorofa10.

Akimuwakilisha   Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt.Samia Suluhu Hassan Mhandisi Masauni amempongeza   Kwa hatua hiyo ya kulitazama Jeshi la Zimamoto Kwa jicho pekee sana nakuongeza Kwa kusema haijawai kutokea Kwa Jeshi hilo kupewa vitendea kazi vya kisasa kama hivyo.

Aidha, Mhe.Masauni kupitia hutuba yake amewataka Askari wa Jeshi hilo kuyatunza Magari hayo ili yadumu kwa Muda mrefu.

Kwa upande wake Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji John Masunga ameipongeza Serikali ya awamu ya Sita Kwa kulijengea uwezo Jeshi hilo .
Post a Comment

0 Comments