TTCL YAZINDUA RASMI HUDUMU YA INTERNET BURE KATIKA VIWANJA HIVI NCHINI

 



Na Mwandishi wetu Dar es Salaam 


Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limetekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan la kutaka uwanja wa Benjamin Mkapa uwekewe huduma ya Mtandao yaani Inteneti ikiwa ni sehemu ya ukarabati katika uwanja huo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo ya Mtandao katika uwanja huo Novemba 5,2023 Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.Nape Nnauye amesema kutekelezwa kwa agizo hilo la Dkt.Samia linakwenda kuwasaidia mashabiki wote wanaoingia kutazama mpira kufurahia kwa kutumia mtandao wenye kasi zaidi.


“Leo tunaanza kuzindua huduma hii ya mtandao wenye kasi katika Uwanja huu wa Mkapa na kwa maagizo ya Rais Samia ni kwamba viwanja vyote vipate huduma ya mtandao ili wanaohudhuria viwanjani wafurahie Mtandao,” amesema Nape


Katika hatua nyingine Mhe.Nape amelipongeza Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) chini ya Mkurugenzi wake Mhandisi Peter Ulanga kwa kufanikisha uwekaji wa huduma hiyo katika uwanja wa Benjamin Mkapa.


“Pigeni makofi ya kutosha kwa TTCL kwa kufanikisha hili la kuweka huduma hii ktaika uwanja huu na naamini kiwanja hiki ni ch kwanza na viwanja vingine vitafuata sasa mnawafanya mashabiki wafurahie kuja uwanjani kwa sababu wanafurahia huduma ya mtandao ambao nimefanyia majaribio na una kasi kwelikweli,”amesema Nape


Nape ameipongeza Azam Media Kwa kuendelea kurusha Matangazo ya mpira Kwa ubora Huku akiamini kuwa uwepo wa Mtandao WA uhakika kutoka TTCL itaendelea kunogesha Matangazo yao.




Post a Comment

0 Comments